RONALDO MOTO WA KUOTEA MBALI, AIPAISHA REAL MADRID DHIDI YA BAYERN MUNICH


Cristiano Ronaldo amefichua makali yake na kuiwezesha Real Madrid kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Hata hivyo ni Bayern waliokuwa wa kwanza kupata bao la pekee ambapo dakika ya 25 Arturo Vidal aliwanyanyua mashabiki wao waliojazana Allianz Arena kwa kutupia mpira wavuni.

Vidal alipoteza nafasi ya kuzima Real Madrid dakika ya 45 baada ya kukosa penalti.

Ndipo ukaja wasaa wa Cristiano Ronaldo kwa kufunga mara mbili katika dakika ya 47 na 77. Timu hizo zitarudiana wiki ijayo kwenye dimba la Santiago Bernabeu.

No comments