Habari

ROONEY AKATA TAMAA MANCHESTER UNITED …aanza kuaga wachezaji wenzake

on

Wayne Rooney anahofia kuwa nafasi yake ndani ya Manchester United inazidi kuwa mashakani na inadaiwa tayari ameshawatonya wachezaji wenzake kuwa atatimka Old Trafford mwishoni mwa msimu.
Rooney mwenye umri wa miaka 31 ambaye huu ni msimu wake wa 13 ndani ya Manchester United, amekuwa akipigwa benchi aidha kwa utashi wa kocha Jose Mourinho au kutokana na kuwa majeruhi.
Mshambuliaji huyo wa England alikosa mechi mbili zilizopita kutokana na kuumia kifundo cha mguu na anatarajiwa kukosa mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht  Alhamisi hii.
Hata hivyo inaaminika kuwa maumivu ya Rooney si makubwa sana na atakubali kucheza mchezo huo iwapo kocha Jose Mourinho atampa nafasi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *