Habari

ROONEY ASEMA BADO ANA MENGI MAZURI YA KUWAPA MANCHESTER UNITED

on

Wayne Rooney amesisitiza kuwa bado ana akiba ya kutosha kwenye uwezo wake wa kutandaza soka na anaamini uzoefu wake unaweza ukaisaidia klabu yake  kumaliza katika ‘top four’ pamoja na kushinda taji la Europa League.
United bado inawinda tiketi ya Ligi ya Mabingwa katika msimu wa kwanza wa Jose Mourinho na tayari ilishanyakua taji  EFL Cup mwezi Februari.
Rooney amesema bado ana makali ya kutosha na ataisadia United kumaliza vizuri sehemu ya msimu iliyosalia.
“Lengo langu ni kuisaidia klabu kwa sehemu iliyobakia, ninaamini nitakuwa msaada mkubwa kwa timu halafu baada ya msimu kukamilika nitajua hatma yangu,” anaeleza Rooney.
Rooney amekuwa akisota benchi kwa sehemu kubwa ya msimu huu ambapo mara nyingi amekuwa akiingia dimbani kama mchezaji wa akiba.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *