SADIO MANE NDO BASI TENA, LIVERPOOL KUMKOSA HADI MSIMU UJAO


Winga wa Liverpool Sadio Mane amefanyiwa upasuaji wa goti, hatua itakayomweka nje ya dimba kwa sehemu yote iliyobakia msimu huu.

Mane aliumia goti lake la kushoto baada ya kugongana na Leighton Baines wakati Liverpool ilipovuna ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo wa Premier League mapema mwezi huu.

Nyota huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 25, alisafiri kwenda London kwaajili ya upasuaji ambapo Jumanne mchana alionekana akitoka hospitalini akiwa na magongo.

No comments