Habari

SAMWEL MSHANA KUAGWA LEO CCM MWINYUMA …mazishi kesho kwao Makanya

on

Mpiga bass wa TOT Band, Samwel Mshana aliyefariki Jumamosi alfajiri,
ataagwa leo mchana katika makao makuu ya TOT – CCM Mwinjuma Mwananyamala jijini
Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa kamati ya mazishi, ratiba ya kuaga mwili wa Mshana,
itaanza saa 7 mchana hadi saa 9 na itakapotimu saa 10 safari ya kwenda Makanya,
mkoani Kilimanjara itaanza.
Mshana atazikwa kwao Makanya kesho mchana.
Kabla ya mwili kupelekwa CCM Mwinjuma, watu watapata mlo wa mchana
kwenye nyumba ya msiba hapo hapo Mwananyamala hatua kadhaa kutoka CCM Mwinjuma.
Mshana ambaye kihistoria, aliibuliwa na Ally Chocky aliyemtoa
bendi ya Fax ya Tanga, alifariki baada ya kulazwa kwa siku tatu katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *