SAMWEL MSHANA “MSHANA BASS” WA TOT BAND AFARIKI DUNIA


Mpiga bass wa TOT Band Samwel Mshana maarufu kama “Mshana Bass” amefariki dunia leo alfajiri.

Mshana (pichani juu) alikuwa amelazwa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa siku tatu zilizopita kufuatia ajali ya pikipiki.

Ajali hiyo ya kushangaza ilitokea Mwananyamala Komakoma  ambapo Mshana akiwa kwenye mwendo mdogo sana kwenye njia mbovu mbovu, aligongana na Bajaj.

Ajali haikuonekana kuwa kubwa na Mshana hakupata majeraha yoyote lakini inadaiwa alipata mshtuko uliomsababishia ganzi au kupooza upande mmoja na kupelekwa Muhimbili alikodumu hadi kifo chake.

Rafiki wa karibu wa Mshana, Ismail Sumaragar ambaye ni meneja wa Mashauzi Classic, ameiambia Saluti5 kuwa marehemu alikuwa kwenye hali nzuri na siku zote alizomtembelea hospital alikuwa mcheshi na hakukuwa na dalili yoyote ya kukatisha tamaa.

No comments