SHABIKI WA TOTTENHAM APEWA KICHAPO CHA MWBWA MWIZI KWA KUDHANIWA NI SHABIKI WA CHELSEA


Ushabiki wa soka usikie hivyo hivyo, kuna watu wana wazimu wa soka na wanaweza kufanya lolote kwaajili ya soka.
Shabiki Tottenham Michael Voller, 23, amepigwa vibaya na mashabiki wenzake wa Tottenham kwa kumdhania kuwa ni mnazi wa Chelsea.
Kichapo hicho kilitokea wiki hii wakati Chelsea ikiitandika Tottenham 4-2 katika mchezo wa nusu fainali ya FA.
Voller ambaye ni mfanyakazi wa zamani wa Tottenham akihudumia uwanja wa mazoezi, alipigwa nje ya mgawaha wa Moore Spice  jirani na uwanja wa Wembley.
Michael Voller aliyekuwa na marafiki zake wakavamiwa na kundi la mashabiki wa Tottenham na kupigwa ngumi za uso akidhaniwa kuwa ni shabiki wa Chelsea.
Ingawa Voller ametoka hospitali, lakini madaktari wanasema anahitaji uangalizi wa karibu na kwamba huenda jicho lake likapoteza uwezo wake wa kuona.


No comments