“SHIKA MOYO” YA IVORY BAND NI MOTO WA KUOTEA MBALI ...Kaa mkao wa kula kuisubiri


Wimbo mpya wa Ivory Band “Shika Moyo” si wa kitoto, ni bonge la songi.

Ngoma hiyo ambayo imesharekodiwa katika studio za Amoroso, ipo katika hatua ya ‘mixing’ na itaachiwa rasmi wiki ijayo.

“Shika Moyo” utunzi wake Rama Pentagon, itasaidia kwa kiasi kubwa kutoa hamasa ya mageuzi ya muziki wa dansi.

Kupitia wimbo huu, Ivory Band wamejivua kabisa kwenye koti la muziki wa rumba na ule masebene makali unaopigwa na bendi nyingi za Kitanzania na badala yake wamekuja na muundo wa kipeke yao.


Ngoma hiyo ambayo Saluti5 imebahatika kuiskia wakati ikirekodiwa,  imepigwa kwa dakika 3 na sekunde 57 na ndani yake hutasikia jina la mtu yeyote atakayerushwa.

Ni wimbo uliojaa utulivu, ujumbe mzuri wa mapenzi na mpangilio bak kubwa wa vyombo. Kaa mkao wa kula kuisubiri nyimbo hii kali.

No comments