SHOLO MWAMBA SASA ATAFUTA "KIKI" ZA KIMATAIFA ZAIDI

MKALI wa Singeli Bongo, Seif Mwinjuma ‘Sholo Mwamba’, amesema kuwa baada ya kukubalika kila kona ya Tanzania, hivi sasa anatafuta njia ya kujitangaza kimataifa kwa kuachia kazi zenye ubora wa hali ya juu zaidi.

Akiongea na ripota wetu jijini Dar es Salaam jana, Sholo amesema kuwa kuvuka mipaka ya nchi kwa muziki wake ndio jambo pekee ambalo hivi sasa analiwazia, huku akidai kuwa anapigana kwa hali na mali kutimiza azma yake hiyo.

“Tangu najitumbukiza kwenye muziki huu, malengo yangu ni kutambulika kimataifa zaidi na sasa najitahidi kuachia kazi zenye ubora unaoweza kupenya na kuvuka hadi mataifa mengine,” amesema msanii huyo.


Amewaomba wasanii wake waendelee kumpa sapoti katika kazi anazozifyatua ili kumjaza moyo na ari ya kuzidi kufanya mambo makubwa katika muziki huo ulioenea kwa kasi hivi sasa hapa Bongo.

No comments