SHOO YA “MSONDO NGOMA FAMILY DAY” LIMEBAKISHA MASAA TU KUANZA KUUNGURUMA BULYAGA TEMEKE

MASHABIKI wa muziki wa dansi maeneo ya Temeke, jijini Dar es Salaam hivi sasa wanahesabu masaa tu kabla ya kuanza kwa shoo kubwa ya Msondo Family pale Bulyaga Bar.

Shoo hiyo inayotazamiwa kujaa msisimko mkubwa inafanyika leo baada ya kusimama kwa muda, tofauti na ilivyokuwa imepangwa kufanyika kila mwezi.

Kiongozi Mwandamizi wa Msondo Ngoma, Said Mabera amesema kuwa kila kitu kiko sawa na kwa upande wao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanamwaga burudani kali kwa mashabiki muda utakapotimia.

Msondo ngoma ni kati ya bendi kongwe za muziki wa dansi, inayokusanya nyota wengi waliowahi kujipatia sifa kutokana na umahiri wao katika aidha uimbaji ama upigaji ala.

Baadhi ya nyota hao ni kama vile waimbaji Shaaban Dede, Juma Katundu, Athuman Kambi pamoja na rapa wao Roman Mng’ande “Romario” ambaye pia ni mpulizaji mzuri wa Tarumbeta.


Wengine ni Abdul Ridhiwan (Gitaa la Solo), Huruka Uvuruge na Jenerali Pishuu (Rithym), James Mawila (Drums).

No comments