SHOW ZA DANSI PASAKA: TWANGA WAKO GIRAFFE, MAPACHA MASAI CLUB, MSONDO BULYAGA TEMEKE, FM DODOMA


Hii ni ratiba ya baadhi ya bendi za dansi kwa sikukuu ya Pasaka leo usiku.

Msondo Ngoma Music Band watakuwa na onyesho maalum la ‘Msondo Family Day’ litakalofanyika New Bulyaga Bar Temeke jijini Dar es Salaam wakati watani zao Sikinde watarindima ndani ya ukumbi wa Teachers Bar, Chamazi Magengeni.

FM Academia wako Dodoma kwenye ukumbi wa Perugina huku Twanga Pepeta wakipiga show ya ‘levo’ za juu ndani ya  Giraffe Hotel.

Mapacha Music Band chini ya Jose Mara itakuwa Meridian Hotel (Club Masai) Kinondoni, Ivory Band wao watapatikana  Champion Night Club, Gongo la Mboto.

Mzee mzima King Kiki na bendi yake ya Wazee Sugu atapatikana Bagamoyo Kaole Snake Park, lakini Original Dar Musica ya Jado FFU itakuwa Friends Corner Hotel Manzese.

Freedom MCB Chikicha chini ya Masoud Kilimanjaro, watawasha moto Chamanzi Pub,  Chamanzi Magengeni.

Kocha wa Dunia Mwinjuma Muumin na bendi yake ya Double M Plus atafanya vitu vyake kwenye ukumbi wa Brazil Pub Tegeta, Mwenge Jazz “Wana Paselepa” watakuwa Dodoma ndani ya ukumbi wa Club La Aziz., Kmondo Music Band nchini ya Richard Mangustino watakuwa Kunduchi Resort Pub, Africana.

No comments