SHOW ZA TAARAB PASAKA: TMK WAKO UKONGA, ISHA MASHAUZI MOMBASA, KHADIJA KOPA KAHAMA, WAKALI WAO MANZESE, MELODY MORO, JAHAZI MBEYA, GUSA GUSA MANGO GARDEN


Hii ni ratiba ya baadhi ya show za bendi kubwa za taarab leo usiku katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

Jahazi Modern Taarab wako mjini Mbeya katika ukumbi wa City Pub wakati East African Melody watakuwa Morogoro ndani ya ukumbi wa Airport Bar.

Mashauzi Classic wanapumzika huku bosi wao Isha Mashauzi akiwa Mombasa, Kenya kwa show maalum ya sherehe za harusi.

Isha alikwea ndege ya Ethiopian Airline leo alfajiri kutoka Dar kupitia Adis Ababa hadi Mombasa na tayari ameshafika salama nchini Kenya.

Ogopa Kopa nao wanapumzika lakini bosi wao Khadija Kopa nae alikwea ndege kwenda Mwanza na baadae kusafiri kwa gari ndogo hadi Kahama ambako leo siku atakuwa na show kwenye ukumbi wa Kikwetu Kwetu Pub.

Wakali Wao Modern Taradance chini yake Thabit Abdul na Khadija Yussuf watapiga show ya kufa mtu kwenye ukumbi mpya ulioko ndani ya hotel ya kisasa Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.

Nao TMK Modern Taarab watapatikana Bwalo la Magereza Ukonga huku Gusa Gusa Mini Band wakifanya yao katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.


No comments