SIMBA SC YAWEKA KAMBI GEITA KUJIANDAA NA MECHI ZA MBAO FC NA TOTO AFRICANS

SIMBA wameweka kambi Geita kujiandaa na michezo yake miwili mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbao FC na Toto Africans.

Kikosi cha Simba kiliwasili jana kwa basi lao kutoka Bukoba, mkoani Kagera ambako juzi walifungwa 2-1 na wenyeji Kagera Sugar.

Kuelekea mechi ya Mbao na Toto, Simba imeamua kwenda kujificha Geita kwa kambi ya maandalizi ili isirudie makosa ya juzi.

Kikiwa mjini Geita, Simba leo ilimenyana na wenyeji Geita Gold katika mchezo wa kirafiki , ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbao.


Katika mchezo wa Mbao FC, Simba itamkosa nahodha wake, Jonas Mkude ambaye anatumikia kadi tatu za njano.

No comments