SIMBA YAHARIBU ‘MIMBA’ YA MBAO FC …maajabu yatokea CCM Kirumba


Ni kama vile mtu alikuwa kubeba ujauzito na kuitunza mimba kwa miezi yote tisa, lakini mambo yakaharibikia hospitali siku ya kujifungua – Mimba ikaharibika.

Mbao FC ya Mwanza iliongoza 2-1 dhidi ya Simba hadi dakika 90 za kawadia zilipomalizika, lakini mwisho wa siku ikakubali kichapo cha 3-2 katika dakika 7 za majeruhi.

Evarigestus  Bernado akaitanguliza Mbao dakika ya 18 kabla George Sangua hajatupia bao la pili dakika ya 33 na kuifanya Simba iende mapumziko katika mchezo huo wa Ligi Kuu ikiwa nyuma 2-0.

Mbao iliyokuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumba – CCM Kirumba, itabidi ijilaumu yenyewe kwa kuamua kutumia mbinu za kujihami pamoja na janja za kupoteza muda.

Wakati Mbao wakiamini kuwa mbinu zao zimezaa matunda, Simba wakafunga bao la kwanza dakika ya 83 kupitia kwa Fredrick Blagnon.

Bao hilo halikuwashtua Mbao na waliendelea na utamaduni ule ule wa kujihami, hatua iliyokaribisha mashambulizi mengi langoni mwao.

Simba wakitumia zaidi pasi ndefu za juu, wakasawazisha dakika ya 92 mfungaji akiwa  Fredrick Blagnon kwa mara nyingine tena.

Dakika ya 96 Simba wakaandika bao la ushindi kwa shuti tamu la Mzamiru Yassin.
No comments