SINGIDA UNITED WAMNASA NDUGU WA HARUNA NIYONZIMA WA YANGA

BAADA ya kufanikiwa kunasa saini za wachezaji watatu wa kiataifa, timu ya Singida United ipo kwenye harakati za kumnasa mshambuliaji wa Polisi ya Rwanda, Danny Usengimana, ili kujiweka sawa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Wachezaji ambao tayari wamenaswa na Singida United ni pamoja na Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn, Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa wote kutoka Dynamos ya Zimbabwe.

Pamoja na kuwepo hali ya kificho katika mchakato wa kumnasa mshambuliaji huyo, taarifa za chini ya kapeti zinadai kuwa Singida United imeshamalizana nae baada ya kumpa mkataba wa miwili.

Danny Usengimana ambaye msimu uliopita alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Rwanda, ataungana na ndungu yake, Haruna Niyonzima anayechezea Yanga.


Singida United imepania kufanya vyema kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao ambapo baada ya kupanda daraja waliamua kufumua benchi lote la ufundi na kumkabidhi kocha mzoefu Hans Pluijim ili kuisuka upya timu hiyo pekee inayowakilisha mkoa wa Singida.

No comments