SIR ALEX FERGUSON ASISITIZA MOURINHO NI CHAGUO SAHIHI MANCHESTER UNITED


SIR ALEX FERGUSON amekiri kuwa bosi wa sasa Manchester United  Jose Mourinho – ndiye alikuwa mtu sahihi kurithi mikoba yake Old Trafford.
'Special One' alikuwa miongoni mwa majina yaliyotajwa kurithi nafasi ya Ferguson mwaka 2013, lakini hatimaye akabahatika David Moyes  ambaye hata hivyo alitumuliwa kabla msimu haujakamilika.
Kwa mujibu wa Daily Mail la Uingereza, Ferguson amekiri kuwa alitaka kocha huyo Mreno amrithi miaka minne iliyopita na kusisitiza kuwa sasa United ina mtu sahihi wa kuirejesha kwenye enzi za mafanikio.

No comments