Habari

SPIDOCH BAND WASIKIE HIVYO HIVYO …UZINDUZI WAO NI MATAWI YA JUU …Next Door yazizima

on

Uzinduzi wa bendi mpya ya Spidoch “Wazee wa Kunena kwa Lugha”,
uliofanyika Jumamosi usiku ndani ya Next Door Masaki jijini Dar es Salaam,
ulikuwa wa matawi ya juu.
Naam ulikuwa wa matawi ya juu kwa namna onyesho hilo lilivyo hudhuriwa
na watu wa matawi ya juu ambao walilazimika kulipa kiingilio cha shilingi
20,000 na 100,000 kwa VIP. Hadhi ya ukumbi nayo ni ya matawi ya juu.
Ukumbi ulishona vizuri, lakini kubwa zaidi ni uhondo uliomiminwa na
bendi hiyo yenye uwezo wa kupiga muziki wa kila aina kuanzia dansi, afro pop na
hata ule wenye vionjo wa kiasili.
Beka Ibrozama staa wa bongo fleva aliyeamua kujitosa kwenye muziki wa
dansi, ndiye rais wa bendi hiyo na kwa hakika alionyesha uwezo wa hali ya juu.
Saluti5 iliyokuwepo ukumbini hapo ilimshuhudia mwimbaji wa zamani wa Mashujaa Band, Pasyaa naye akitisha kwa namna
sauti yake tamu ilivyokuwa ikipenya kwenye ‘sound’ bab kubwa ndani ya Next
Door.
Rapa wa kinyakyusa Power Bank aliyekuwa akishambulia jukwaa huku
ameshika kigoda mkononi, alikuwa ni msanii mwingine wa Spidoch aliyeuteka
ukumbi.
Spidoch imeenea vizuri na hakukuwa na eneo lililokuwa na dalili ya
kupwaya na kama una penda bendi zenye kupiga pamba kali, basi huenda Spidoch
wakawa hawana mpinzani na kama wewe ni mpenzi wa masauti basi Spidoch Band
watalifikisha sikio lako kule kunakostahili.
Moja ya wimbo uliotingisha Next Door ni wimbo “Mtu Kwao” ambao ulikuwa na kila kitu kinachohitajika kwenye dansi la kisasa.
Kama bendi hii itadumu kama ilivyo, basi Tanzania itakuwa imeingiza
ingizo la maana kwenye soko la muziki.
 Beka Ibrozama akitona neno la shukrani kwa katibu wa Chamuda Hassan Msumari (katikati). Kulia ni mtangazani Ben Kinyaiya
 Ben Kinyaiya aliyekuwa MC, aliutendea haki uzinduzi wa Spidoch
Rapa Power Bank akicheza na kigoda chake mkononi
 Madansa wa Spidoch wakishambulia jukwaa
 Hakika Spidoch walitesa kwa sana
Waimbaji wa Spidoch wakiwa kwenye pamba kali

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *