SPIKA WA BUNGE AWADHIHAKI YANGA KWA KUWAITA "4G"

SPIKA wa bunge la Jamhuli ya Muungano wa Tanzania, mh. Job Dungai juzi katika kikao cha bunge aliwatupia dongo Yanga ambao mwishoni mwa wiki iliyopita walichalazwa mabao 4-0 na MC Alger ya Algeria na kuendeleza utani kwa mashabiki kwamba wamekuwa watu wakupigwa “4G” kila mara.

Yanga imetolewa nje ya mashindano ya Kombe la Shirikisho ambako iliangukia pua baada ya kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika na Zanaco FC ya Zambia.

Spika wa Bunge alisema kwamba bora hamasa kubwa ielekezwa kwenye sanaa kwa sababu kwenye soka kuna matatizo.

Katika kikao cha Bunge la bajeti kilichofanyika Jumanne mkoani Dodoma, Spika Dungai alitupa dogo hilo kwa kusema.

“Namuunga mkono Naibu Waziri kwamba tukazanie mambo ya sanaa, maana inaelekea mpira wa miguu unatushinda kidogo,” akasema Spika Ndugai, kisha akaendelea.

“Watu wamepoteana uwanjani bao 4-0, wakapoteana mjini wakarudi mafungu mafungu, namuuliza mheshimiwa Waziri Mkuu vipi anasema hata sielewi kinachoendelea."

Yanga walisafiri kwenda Algeria kwa mafungu ingawa walikuwa na ushindi wa bao 1-0 walioupata jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.

Lakini hata baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya aibu nchini humo, baadhi ya viongozi wa Yanga walichelewa kurejea nchini kwa kile kilichotajwa kwamba walichelewa ndege na mitandao mingine ikisema kwamba Yanga walipotea njia.


Hata hivyo, hoja ya kupotea njia imekuwa nyepesi kwasababu Yanga hawakuwa wanakwenda wenyewe uwanja wa ndege, bali walikuwa wanaongozwa na mwenyeji, labda kama waliamua kutembea kwa miguu kutoka hotelini hadi uwanja wa ndege, jambo ambalo nalo linazua maswali mengi. 

No comments