STAA WA MUZIKI NIGERIA ASHAMBULIWA NA MASHABIKI KWA KUCHOCHEA KUWAGAWA P-SQUARE

STAA wa muziki nchini Nigeria, Timaya ameshambuliwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana mchochezi anayetaka kuligawa kundi la mapacha la P Square.

Nyota huyo anayetamba na kibao chake cha “I Concur” aliposti kwenye mtandao juu ya mpango wake wa kufanya nyimbo na Paul, moja kati ya memba wa P Square.

“Nitafanya nyimbo na Paul kwasababu naamini ndie mwanamuziki bora kwa kizazi cha sasa,” ilisomeka sehemu ya posti kwenye akaunti yake ya Instagram.

Baada ya posti yake, alikumbana na majibizano toka kwa mashabiki ambao walimponda na kumuona kama mtu anayetaka kulisambaratisha kundi lao.


“Usiigawe familia hiyo, Peter hana mpango wa kazi unayotaka kufanya na Paul, lakini tafadhali usiwe mchochezi,” ilisomeka moja ya kati ya komenti zilizotumwa.

No comments