SUPER NYAMWELA WA TWANGA PEPETA ATIMKIA OMAN


Dansa gwiji wa muziki wa dansi Super Nyamwela anayeitumikia Twanga Pepeta, mapema leo alipaa kwenda Oman kwa shughuli za kimuziki.

Akiongea na Saluti5 muda mfupi kabla hajapaa na ‘pipa’ la Emirates, Nyamwela akawataka mashabiki wake na wa Twanga kwa ujumla wasiwe na shaka kwani ziara yake ni ya wiki mbili tu.

“Nimeitwa Oman kwa kazi ya wiki mbili, kama kutatokea mabadiliko nitakujulisha, lakini makubaliano yangu ni ya wiki mbili,” alisema Nyamwela.
Super Nyamwela ndani ya ndege ya Emirates akielekea OmanNo comments