TETESI ZA KUACHANA KWA HARMONIZE NA JACK WOLPER ZAGEUKA GUMZO... Babu Tale agoma kuzungumzia

WIKI lote hili kumekuwa na taarifa ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kuvunjika kwa penzi lililonoga baina ya mastaa wawili; Jackline Wolper ambaye ni mcheza filamu na rapa Harmonize.

Harmonize ambaye ni staa wa wimbo “Matatizo” anadaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na dada wa kizungu, huku taarifa zikidai kuwa tayari ameshampa ujauzito.

Nae meneja wake, Babu Tale hakutaka kuzungumzia hili ambapo alidai kuwa kazi yake ni kusimamia sanaa tu na sio mapenzi ya wasanii.

“Sio kazi yangu kuzungumzia masuala ya mahusiano yao, kazi yangu ni kusimamia biashara ya muziki tu, sisimamiaa masuala yao ya mapenzi,” alisema Babu Tale.


Wolper na Harmonize tangu mwanzo wa penzi lao walikuwa wakishambuliwa na wadau mbalimbali, huku baadhi ya watu wakihoji tofauti yao ya umri ambapo Wolper akionekana kuwa na umri mkubwa zaidi.

No comments