Habari

THEO BONGONDA AITOA UDENDA MANCHESTER UNITED

on

Mshambuliaji  wa Celta Vigo,  Theo Bongonda amefungua milango kwa usajili wa dirisha la kiangazi kwa kusema anaamini kuwa yupo tayari kwa kuzitumikia timu kubwa barani Ulaya.
Kinda huyo wa miaka 21, ameonyesha uwezo mkubwa kwenye La Liga na tayari amezivutia timu kadhaa ikiwemo Manchester United.
Inaaminika United imeshatuma maskauti wake mara kadhaa kwenda kuangalia kiwango cha Bongonda.
Alijiunga na Celta akitokea Zulte-Waregem mwaka 2015 na sasa amebainisha kuwa hana dhamira ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Hispania.
“Ninaweza kuwa radhi kubakia Vigo kwa miaka miwili au mitatu, lakini sio dhamira yangu kumalizia soka langu hapa,” Bongonda aliwaambia waandishi wa habari.
“Kama Manchester United, Chelsea au Atletico Madrid  watahitaji huduma yangu hapo baadae, sitasita kujiunga nao.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *