TOTO AFRIKA YAIKAZIA SIMBA …ubingwa bao hauna mwenyewe


Simba Sports Club imedhihirisha kuwa bado sio timu yenye uchu wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africa ya Mwanza.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanza wa CCM Kirumba Mwanza, Simba walikosa kabisa maarifa ya kuzigusa nyavu za Toto na mara kadhaa walinusurika kufungwa wao.

Katika mechi mbili ziliozipita Simba imeonyesha kiwango cha chini ambapo ilikubali kichapo cha bao 3-1 kwa Kagera Sugar (ingawa baadae walivuna ushindi wa mezani), wakapata ushindi wa mbinde 3-2 kwa Mbao FC ya Mwanza pale walipolazimika kusubiri hadi dakika za nyongeza kupata mabao mawili ya haraka haraka.

Kama Yanga inayoshika nafasi ya pili itashinda mechi zake za viporo, basi itafikisha pointi 62 sawa na Simba.

No comments