TOTTENHAM YAFANYA MAAJABU YA MSIMU NDANI DAKIKA TATU ZA MWISHO DHIDI YA SWANSEA


Tottenham wameifanyia kitu mbaya Swansea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwa kuichapa kichapo cha maajabu.

Tottenham ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Jordan Ayew kunako dakika ya 17, lakini wakafunga magoli matatu ya haraka haraka ndani ya dakika tatu za mwisho wa mchezo wafungaji wakiwa ni Christian Eriksen, Heung-Min Son na Dele Alli.

Matokeo ya mechi zote za Premier League zilizochezwa Jumatano usiku ni haya hapa:
Arsenal 3 - 0 West Ham United
Hull City 4 - 2 Middlesbrough
Southampton 3 - 1 Crystal Palace
Swansea City 1 - 3 Tottenham Hotspur
Chelsea 2 - 1 Manchester City
Liverpool 2 - 2 AFC Bournemouth
No comments