TOTTENHAM YAIBANJUA BOURNEMOUTH 4-0 NA KUVUNJA REKODI YAO YA MIAKA 50


Ni miaka 50 tangu Tottenham ishinde mechi saba mfululizo za ligi - nusu karne na sasa ni wazi kuwa wanaelekea kumaliza ligi juu ya watani zao wa London, Arsenal kwa mara ya kwanza baada ya miaka 22.

Tottenham inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu imeichapa Bournemouth 4-0 na kuzidi kupunguza pengo la pointi kati yake na vinara Chelsea.

Magoli ya Tottenham yalifungwa na Moussa Dembele, Heung-Min Son, Harry Kane na Vincent Janssen katika dakika ya 18, 19, 48 na 90

No comments