UKAME WA MABAO UNITED WAMFANYA MOURINHO KUUKUMBUKA MGUU WA CHICHARITOTANGU Javier Hernandez maarufu kama “Chicharito” auzwe kwenda Bayer Leverkusen ya nchini Ujerumani, maisha yake kisoka yamebadilika sana na kasi yake ya ufungaji imekuwa kubwa sana kiasi kwamba kila mtu anamzungumzia.

Wakati Chicharito akiwa anafunga sana magoli huko aliko inaonekana tatizo la ufungaji ndani ya United halijapata tija bado kwani pamoja na kufunga sana lakini Zlatan Ibrahimovic anaongoza klwa kupoteza nafasi.

Kocha Jose Mourinho analijua hilo na akakiri kwamba kama mtu aina ya Chicharito angekuwepo ndani ya Manchester United basi hadi hivi sasa angekuwa ameshafunga magoli zaidi ya 20.

Chicharito hakuwa na bahati ndani ya United lakini bado ni kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo, michezo mingi aliyoingia akitokea benchi alifunga magoli muhimu lakini Van Gaal alimuuza huku mashabiki wakiwa bado wanamtaka.

“Nataka nikupe mfano kwa jinsi tunavyocheza mpira na kwa jinsi tunavyoshambulia hadi sasa Chicharito angekuwa na magoli 20 au zaidi, hata kama angecheza kwa dakika kumi au 20 tu za mwisho, ni mchezaji ambaye akiwa ndani ya boksi anahakikisha mpira unaenda kambani,” alisema Mourinho.

Mourinho anasema sio kwamba wachezaji wake wabaya, bali hawana ile hulka ya uuaji wa magoli kama ilivyo kwa Chicharito.


Mourinho anaona nafasi ambazo Pogba amegongesha mwamba, mtu kama Chicharito angeitumia mipira hiyo inayotoka kugonga mwamba kuweza kufunga, haijaeleweka kama United wanataka kumrudisha klabuni hapo au vipi.

No comments