USAJILI WA KWANZA WA ARSENAL HUU HAPA ...bonge la beki kutoka Schalke


Arsenal imekamilisha dili la kumnasa beki wa kushoto wa Schalke,  Sead Kolasinac  kwa usajili huru, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Bosnia zilizodakwa na mtandao wa Daily Mail wa Uingereza.
Kolasinac  amekuwa kwenye rada za Wenger kwa muda mrefu na anatarajiwa kwenda kupigania namba na Nacho Monreal.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyeichezea timu ya taifa ya Bosnia mechi 18, aliwaniwa na Chelsea bila mafanikio dirisha la mwezi Januari wakati Manchester City, Juventus na Liverpool zote zilikuwa zikimwinda.

No comments