VICTOR LINDELOF ANUKIA TENA KUSAJILIWA MANCHESTER UNITED


Inaonekana kama vile Manchester United itafanikiwa kumsajili sentahafu wa Benfica Victor Lindelof anayewaniwa pia na Roma ya Italia.
Ripoti zinadai United imeshafanikiwa kufanya makubaliano ya awali na nyota huyo wa kimataifa wa Sweden.
United ilijaribu kumsajili Victor Lindelof bila mafanikio katika dirisha dogo la mwezi Januari, lakini safari inaelekea samaki amenasa chambo.

No comments