VIDEO: JIKUMBESHE WIMBO “SHAMBA LA BIBI” WA VICTORIA SOUND YA MWINJUMA MUUMIN


Moja ya vikosi ambavyo kufa kwa kwake ilikuwa ni pigo kwa muziki wa dansi ni Victoria Sound iliyokuwa chini ya Mwinjuma Muumin mwaka 2014.

Bendi hii iliyokuwa na nyota kadhaa kama Muumin, Waziri Sonyo, Januari Eleven, Dogo Hijja (Muumin Junior), Sele Mumba, Mussa Karenga na wengine wengi ilitisha sana kupitia wimbo wao  wa “Shamba la Bibi”.

Wimbo huu uliibuka kuwa gumzo la jiji hasa kutokana na madongo yaliyosukumizwa ndani yake lakini pia kwa namna ambavyo kila msanii aliyeshiriki aliutendea haki.

Jikumbushe video hiyo ya “Shamba la Bibi” iliyokuwa majibu mubashara kwa wimbo “Shamba la Twanga” wa Twanga Pepeta.

No comments