VITA YA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA YAPAMBA MOTO LIGI KUU TANZANIA BARA

MZUNGUUKO wa pili Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwa ukingoni, vita ya kupigania kutoshuka daraja inaonekana kuziganda timu nne za chini ambazo ni Majimaji ya Songea, JKT Ruvu, Ndanda na Toto African ambayo iliilazimisha Simba sare kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ndanda inapumua kidogo kwa sababu ya kuwa juu kwa pointi nne zaidi ambapo imejikusanyia jumla ya pointi 30 huku Majimaji na Toto African wakifungana kwa kuwa na alama 26.

Hali ni mbaya zaidi kwa JKT Ruvu wanokamata nafasi ya mwishi wakiwa na alama 23.

Hata hivyo timu ya Ndanda ambayo walau ina usalama imetangulia mbele kwa mchezo mmoja zaidi wakicheza mechi 27 ambapo timu ya Toto African wakiwa na michezo 26.

Timu hizo zitarudi tena Mei 6 zikipigania pointi za kutoshuka daraja wakati ambapo Ligi kwa sasa inaelekea ukingoni na mbio za ubingwa zimebaki mikonono mwa timu mbili sza Simba na Yanga.


Yanga ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligi hiyo ikiwa atafanikiwa kubeba Kombe litakuwa mali yake baada ya kufanya hivyo kwa msimu mitatu mfululizo.

No comments