WAARABU WA MC ALGER WAMTAMANI OBREY CHIRWA WA YANGA

YANGA imewachapa Waarabu wa MC Alger ya Algeria juzi kwa bao 1-0 lakini utamu zaidi ni usajili ambao Waaarabu hao wanataka kufanya kwa kumtengea kiasi cha sh mil 200 mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa.

Chirwa ambaye ndiye aliyetoa pasi ya bao la Kamusoko alionekana kuwasumbua mabeki wa Algeria na mara baada ya mchezo huo kumalizika Waarabu hao walimfuata Chirwa na kuteta naye kwa sekunde kadhaa.

Aliyeteta na Chirwa ni kocha msaidizi wa timu hiyo, Meguelati Abdelhak ambaye alionekana kufanya siri kile walichokuwa wakiteta na Chirwa ambaye bado ana mwaka mmoja katika mkataba wake na Yanga.

Kocha mkuu wa MC Alger, Moussa Kamel aliiambia Saluti5 juu ya kumkubali Chirwa akivutiwa na kujua kuitumia akili yake katika kutafuta mabao ambapo alikuwa mwiba kwao.

Kamel alisema Chirwa alionekana mapema kuwa tatizo kubwa ambalo alilazimika kuwapa majukumu mabeki wake kuwa makini na Mzambia huyo ili asilete madhara.

“Ni mshambuliaji mzuri na ana akili nyingi, msumbufu lakini pia anajua kutumia nguvu zake vyema, alikuwa ni hatari zaidi kwetu,” alisema kocha huyo.

“Nimeagiza viongozi wafanye harakati kuangalia kumpata, sijajua sheria za hapa zikoje katika kusajili lakini kama timu yake itakubali tutawapatia kiasi kizuri.”

Taariifa zaidi ni kwamba Walgeria hao wapo tayari kutumia kiasi cha sh mil 200 kuhakikisha Chirwa anatua mji wa Maloudia katika kusajiliwa.


Kipa namba moja wa timu hiyo, Chaouchi Fawzi amepigilia msumali mawindo hayo akisemani bahati kwao kutoka bila kufungwa na mshambuliaji huyo ambaye alikuwa hatari katika muda wote wa mchezo.

No comments