AC Milan ya Italia imeuzwa kwa kampuni moja ya China na kuhitimisha umiliki wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo,  tajiri Silvio Berlusconi.
Kampuni ya China Rossoneri Sport Investment Lux, imekamilisha mkataba wa kuinunua timu hiyo kwa kima cha dola milioni 628, huku ikiwa na matumaini ya "kuongeza faida mara dufu".
Klabu hiyo ya Serie A imekuwa chini ya umiliki wa bilionea Silvio Berlusconi, tangu mwaka 1986.
Katika kipindi hicho chote, AC Milan ilifaulu kunyakua mataji manane katika ligi kuu na kunyakuwa kombe la vilabu bingwa barani Ulaya mara tano.
Aidha, Milan haijawahi kushinda mechi za Seria A tangu mwaka 2011 na imemaliza katika nafasi ya 7, 10 na 8 katika misimu mitatu iliyopita.
Kwa sasa inashikilia nafasi ya 6 katika ligi kuu, alama 20 nyuma ya vinara Juventus.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac