WANACHAMA WA YANGA WAKITAKA KIKOSI CHA TIMU YAO KUTETEA UBINGWA WA LIGI KUU KWA HALI NA MALI

WANACHAMA wa Yanga wamekipa kikosi hicho kazi ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ili kulinda heshima ya klabu.

Yanga imetolewa kjwenye Kombe la CAF na inakabiliwa na michuano ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA ambapo Jumamosi ya wiki hii watacheza dhidi ya Prisons ya Mbeya.

“Tunajua kuna matatizo ya fedha kwasababu timu inapitia kipindi cha mapito lakini kwa heshima ya klabu tunaomba wachezaji watuletee ubingwa,” alisema moja kati ya wanbachama hai wa Yanga.

“Wachezaji wanahitaji kuwa wazalendo kwa klabu yao, umoja unajhitajika kwa nyakati zote za shida na raha, itakuwa jambo jema kama watapambania ubingwa msimu huu,” aliongeza.

“Yanga ni klabu kubwa hivyo masuala ya fedha yatapatiwa ufambuzsi tu ni suala la kusubiri tu.”


Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wapo kwenye kipindi cha mpito na kumekuwa na taarifa za baadhi ya wachezaji kuwa na mgomo wakishinikiza kulipwa madai yao.

No comments