Habari

WANAYANGA WENYE MACHUNGU YA POINTI TATU ZA CHEE ZA SIMBA WAZIDI KUONGEZEKA MAHAKAMANI KISUTU

on

KIONGOZI wa tawi la Yanga
Tandale jijini Dar es Salaam maarufu kwa jina la “Jitu” ameungana na mwanachama mwingine nguli, Sud Tall ili kwenda mahakama ya Kisutu kusimamisha Ligi Kuu
Tanzania Bara.
Wanachama hao nguli wa klabu ya Yanga wanapinga mazingira yaliyotumika kuipa Simba pointi 3 na mabao 3 kutokana
na rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar.
Simba iliyopewa pointi hizo na Kamati ya saa 72 baada ya kupinga Kagera Sugar kumtumia Mohamed Fakhi katika
mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba na kufungwa mabao 2-1.
Kamati ya Ligi ya saa 72 ilitoa
uamuzi huo mapema Alhamisi wiki iliyopita ambapo hata hivyo uamuzi huo
umepingwa vikali na viongozi wa Yanga na hata klabu ya Kagera haijaafiki kupokwa pointi hizo.
“Hakuna jambo lisilokuwa na
mwisho, nimepanga kuungana na Tall mahakamani Kisutu leo kusimamia Ligi mpaka
pale suala hili litakapopatiwa ufumbuzi,” alisema mwanachama huyo hai wa Yanga.
“Ndiyo, kuna mazingira ya utata ya namna ambavyo Simba wamepewa pointi za chee, ngoja tuone mahakama itasema nini, pointi
za mchezo wa soka zinapatikana uwanjani na sio mezani kama walivyofanya
wenzetu,” aliongeza.

Klabu ya Yanga inakamata nafasi
ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya Simba ambao Jumamosi walicheza
na Toto African katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *