Habari

WASHAMBULIAJI WA MANCHESTER UNITED WAMCHEFUA MOURINHO

on

Jose Mourinho ameuponda mchango wa washambuliaji wake baada ya Manchester United kubanwa kwa sare tasa kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Premier League uliochezwa Jumamosi.
Nyota wa bei mbaya Anthony Martial na Henrikh Mkhitaryan, pamoja na machipukizi waliokulia Manchester United  Marcus Rashford na Jesse Lingard walimchefua kocha huyo baada ya kusababisha sare ya nane msimu huu ndani ya  Old Trafford.

TWAKWIMU ZA WASHAMBULIANI WA MAN UNITED – 2016-17 SEASON

Anthony Martial
Michezo: 29
Magoli: 7
Henrikh Mkhitaryan
Michezo: 27
Magoli: 8
Marcus Rashford
Michezo: 38
Magoli: 7
Jesse Lingard
Michezo: 27
Magoli: 5
Mourinho amesema wachezaji hao wanne walipoteza mwendelezo wa umakini. “Siku moja wanaweza kuwa wazuri na siku nyingine wakawa chini ya kiwango,” alisema Mourinho na kudai kwa timu kubwa inayohitaji kushinda mataji lazima mchezaji adumishe ubora wake kila siku.
“Kwa dakika 90, Antonio Valencia alikuwa timamu, Marcos Rojo, Eric Bailly, Ashley Young, Marouane Fellaini, Michael Carrick nao walikuwa katika ubora wao. Lakini waliobakia walikuwa chini ya kiwango,” anaeleza Mourinho
“Ukitazama rekodi zetu za magoli unaweza ukadhani tunacheza kwa kujihami au ni timu inayoshambulia kwa kuvizia lakini sivyo kabisa. Tunatawala mpira, tunashambulia kwa muda mwingi lakini tunashindwa kuwaangamiza wapinzani wetu.


“Rashford, Lingard, Mkhitaryan, Martial, tazama magoli yao waliyofunga.  Zlatan na [Juan] Mata ndio pekee wenye magoli mengi. Bila wao tungekuwa kwenye hali ngumu zaidi,” anafafanua Mourinho.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *