WASHAWASHA CLASSIC KAMA KAWA FRIENDS CORNER MANZESE ARGENTINA

WAPENDA maraha wa kitongoji cha Manzese na maeneo jirani, kama ilivyo ada leo Alhamisi wanatarajiwa kumiminika ndani ya Friends Corner, Manzese Argentina, Dar es Salaam pale kundi la taarab la Washawasha Classic Min Band litakapokuwa likiunguruma.

Bosi wa Washawasha Classic, Amour Maguru ameitonya saluti5 kuwa, burudani ndani ya ukumbi huo itaanza majira ya saa 12:30 jioni ambapo amewaomba mashabiki kufika kwa wingi ili kujipatia mambo matamu ikiwemo vibao vyao vipya ambavyo ni maandalizi ya albamu yao ya kwanza.

“Tutakuwa na surprise kibao katika shoo yetu ya leo, hivyo tunawaomba mashabiki pamoja na wapenzi wetu wote waje kwa wingi ili kushuhudia na kupata kile ambacho tumekiandaa kwa ajili yao,” amesema Amour ambaye ni kati ya wapapasaji kinanda mahiri wa taarab hapa Bongo.


Washawasha Classic ni kati ya bendi za taarab zilizoko juu kwa sasa kutokana na kukubalika vilivyo kwa mashabiki wa miondoko hiyo, hasa kwavile inakusanya mastaa wenye wapenzi wengi wakiwemo Mwanahawa Chipolopolo, Omary Sosha na Super Amran.

No comments