WASHAWASHA CLASSIC, MUUNGANO CULTURE TROUPE WARINDIMISHA MUZIKI NA JUA KALI

KWA mujibu wa ratiba ya bendi ya taarab ya Washawasha Classic Min Band wanaotumbuiza ndani ya ukumbi wa Friends Corner Hotel, Manzese leo, saa hizi tayari moto umeshawaka.

Washawasha wanatumbuiza ukumbini hapo sambamba na bendi iliyowahi kuwa tishio kubwa huko nyuma, ambayo hivi sasa imerejea upya ya Muungano Cultural Troupe chini ya mkali wa kucheza na nyoka, Norbert Chenga.

Bendi hizo mbili zitatumbuiza kwa zamu kuanzia muda huo hadi saa 5:00 usiku itakapokuwa mwisho rasmi wa burudani.


Hii ni mara ya kwanza kwa bendi za taarab kutumbuiza mchana ukumbini, baada ya miaka mingi kupita, wakati ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni kipindi ambacho TOT na Muungano zilikuwa kwenye ubora wao.

No comments