PICHA 8: WASHAWASHA WAZIDI KUMIMINA BURUDANI YA NGUVU FRIENDS CORNER, MANZESE ARGENTINA

BENDI changa ya mipasho lakini inayoonekana kukubalika vilivyo kwa mashabiki, Washawasha Classic Min Band, Alhamisi hii imeonekana kuendelea kuujaza vilivyo ukumbi wa Friends Corner ulioko Manzese Argentina, jijini Dar es Salaam.

Mamia ya mashabiki waliohudhuria shoo ya jana, walionyesha shamrashamra za aina yake kudhihirisha kuwa wamezidi kuukubali “mziki” wa Washawasha iliyo chini ya mpapasa kinanda mahiri, Amour Maguru.

Wasanii wa bendi hiyo, wakiwemo waimbaji Mwanahawa Chipolopolo, Omary Sosha, Super Amran na Semeni walizidi kukoleza mcharuko wa mashabiki wao, hasa kutokana na kuimba vibao vilivyoonekana kuwasuuza mno mioyo yao. 

Pata picha 8 hapo chini za namna shoo ilivyokwenda.

Safu ya waimbaji wa kike wa washawasha Classic wakimwaga raha kwa mashabiki wao
Mwimbaji Semeni akikonga nyoyo za mashabiki jukwaani
Hapa mkali wa wimbo "Yamenichosha Maumivu" Super Amran akiwachizisha wapenzi wao

Amour Maguru akipapasa kinanda kwa umakini mkubwa

 Malkia wa Washawasha Classic, Mwanahawa Chipolopolo nae akiimba kwa mbwembwe
 Mpapasa kinanda Shaaban Wakumwaga akiwa kazini
 Hapa raha za burudaniu ya Washawasha Classic zinaendelea
 Omary Sosha akiimba kwa hisia kali

No comments