WAZIRI MKUU MAJALIWA AIPONGEZA SERENGETI BOYS KWA TIKETI YA KUSHIRIKI AFCON

WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameipongeza timu ya taifa ya Vijana “Serengeti Boys” kwa kupata tiketi ya kushiriki kwenye michuano ya Afcon nchini Gabon.

 Mtendaji mkuu huyo wa shughuli za serikali amempongeza pia mwanariadha wa mbiao ndefu wa Tanzania aliyeshinda medali ya dhahabu hivi karibuni huko nchini India Alphone Simbu ambaye amefungua njia ya kufanya vizuri zaidi kwa wanariadha wengine na kuirudisha Tanzania katika ramani ya mchezo huo ulimwenguni kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

Pia Mheshimiwa Waziri Mkuu aliwapongeza pia timu ya taifa ya wanawake “Twiga Stars” kwa kuwa mabingwa wa Kombe la Afika mashariki na Kati (CECAFA).                                                                                                            
Waziri mkuu alitoa taarifa hiyo wakati alipokuwa akiwasilisha bajeti ya makadilio ya wizara yake mjini Dodoma.

Amewataka wadau mbalimbali nchini kuisaidia timu ya taifa ya vijana kwa hali na mali ili iweze kufanya vyema kwenye michuano ya Afcon nchini Gabon lakini pa iweze kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini India.


Serengeti Boys ambao wamepaa juzi kuelekea nchini Morocco kuweka kambi ya mwezi mmoja, waliangwa na makamu wa rais, Samia Suluhu ambaye aliwaandalia chakula cha pamoja na kuwataka wakalipiganie taifa.

No comments