WAZIRI MWAKYEMBE AUITA UONGOZI WA SIMBA NA KUTETA NAO OFISINI KWAKE

UONGOZI mzima wa klabu ya Simba jana umefanya kikao na waziri mwenye dhamana ya michezo Dk. Harrison Mwakyembe mjini Dodoma.

Taarifa ya Wiziri ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kupitia ukurasa wake wa facebook jana imesema kwamba Mwakyembe alikutana na uongozi wa timu ya Simba ukiongozwa na rais wake, Evans Aveva kwenye ofisi ya waziri Dodoma.

Taarifa hiyo imesema kwamba uongozi wa Simba uliitikia wito wa waziri Mwakyembe wa kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maendeleo ya uendeshaji wa timu.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu mkuuu wa waziri, mkurugenzi wa michezo wa wizara, Katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania BMT na msajili wa klabu na vyama.

“Mhe Mwakyembe alipokea maoni ya kiongozi wa Simba na ushauri ili kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu hapa nchini,” imesema taarifa hiyo.


No comments