WEMA SEPETU: HARMORAPA ACHA KUTAFUTA KIKI KUPITIA MGONGO WANGU

STAA wa filamu nchini anayeongoza kwa kupamba vichwa vya magazeti nchini Wema Sepetu amemtaka chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Harmorapa kuacha mara moja kumchafulia jina lake mbele ya jamii iliyomzunguka.

Harmorapa aliwahi kuposti kwenye akaunti yake ya Instagram na kueleza namna anavyomzimia modo huyo huku akijihasibu kumudu gharama zake.

Akizungumza, Wema Sepetu alimtaka Harmorapa kuacha kumchafua kwenye vyombo vya habari kwa kutumia jina lake kama kiki ya kutokea kimuziki.

“Sipendi kufanya marumbano na mtu yeyote kupitia mnitandao ya kijamii na vyombo vya habari, niko bize nikifanya mambo yangu hivyo namtaka Harmorapa haachana na mimi,” alisema Wema.


Harmorapa pia alianzisha vita ya maneno na dansa wa lebo ya Wasafi, Moze Iyobo aliye chini ya Diamond huku akielezwa kuwa sehemu ya kutafuta kiki kimuziki.

No comments