WENGER ASEMA ARSENAL LAZIMA IFANYE USAJILI MKUBWA MSIMU UJAO


Kocha wa Arsenal - Arsene Wenger anasema kuwa ameanza kupanga safu ya wachezaji atakaonunua msimu ujao licha ya kuwa hajapata thibitisho kwamba atasalia katika klabu hiyo.

Mkataba wa Wenger unaisha mwisho wa msimu huu na tayari mezani mwake amepewa mkataba mpya ya miaka miwili lakini bado hajaamua lolote.

''Nafanya kazi hadi siku ya mwisho ya msimu'', alisema Wenger mwenye umri wa miaka 67 na kuongeza ''Wachezaji watakanunuliwa ndio taswira ya kila klabu katika siku zake za usoni'' .

''Swala la iwapo nitasalia au la sio muhimu kwa sasa, lakini nina maeneo katika timu ambayo yanahitaji wachezaji wapya. Arsenal ni lazima ifanye usaji mkubwa.”

No comments