WENGER ASEMA HATMA YAKE HAITAATHIRI WACHEZAJI WA ARSENAL


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, anasema kuwa hatma yake ya baadaye ndani ya Emirates haitawatatiza wachezaji kwa namna yoyote ile.
Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu huu, huku kukiwa na ofa mezani ya kandarasi mpya ya miaka mingine miwili.
Hata hivyo Wenger bado hajatangaza iwapo ataendelea kuifunza Arsenal au la.
Wakati Wenger akiendelea kupiga kimya juu ya hatma yake, mashabiki wa Arsenal wamegawanyika ambapo baadhi wanataka atimke huku wengine wakisema bado wana imani nae.
Arsenal iliyo katika nafasi ya 6, iko na alama saba nyuma ya timu nne zilizoko katika nafasi za kwanza, huku ikisalia na mechi nane tu kukamilisha msimu huu.
"Nimeiongoza Arsenal katika mechi 1,100, na hatujawahi kushindwa namna hii," amesema mfaransa huyo.
“Watu wanahoji juu ya hatma yangu na baadhi ya wachezaji nyota, sioni kama vitu hivi viwili vinahusiana. Hatma yangu haitaathiri wachezaji kwa namna yoyote ile,” anaeleza Wenger.

No comments