WENGER ASEMA UCHEZAJI IMARA NDO KIBOKO YA WAKOSOAJI WANOKO

Arsene Wenger amesema dawa ya wakosoaji wenye makuu ni Arsenal kuwa na uchezaji imara uwanjani sambamba na kuvuna ushindi.
Wenger amesema ushindi ndo silaha pekee ya kuwafunga midomo wakosoaji na hivyo amewataka wachezaji wake kuendeleza moto waliouonyesha kwenye mchezo wa FA dhidi ya Manchester City uliowapa ushindi wa bao 2-1 na kutinga fainali.
Hii inakuwa mara ya 20 kwa Arsenal kufika fainali, na mara ya nane chini ya Wenger.
"Watu walitilia shaka uwezo wetu, tulipitia wakati mgumu," Wenger alisema.
"Mnaweza kutengana au kuwa na umoja na tulitoa jibu sahihi."
baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakiandamana dhidi ya meneja huyo miezi ya karibuni.

"Ninahisi kwamba klabu hii imo katika hali nzuri, na kwamba kwa jumla tuna kikosi imara," alisema.
Arsenal inajitupa uwanjani leo usiku katika mchezo wa Premier League dhidi ya Leicester City.

No comments