WENGER ASISITIZA SANCHEZ HAUZWI ENGLAND


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amezidi kusisitiza kuwa kamwe hatomuuza Alexi Sanchez kwa vilabu pinzani wa Premier League.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Chile, ambaye alifunga bao la ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Manchester City ana mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wake Arsenal nab ado hajaonyesha nia ya kuendelea kubaki Emirates.

''Sidhani kama unaweza kumuuza kwa klabu yoyote ya Uingereza, huo ni ukweli'', alisema Arsene Wenger na kuongeza: ''Lakini kama nilivyosema, nadhani atasalia na kuweka saini mkataba mpya''.

Wenger bado hajathibitisha iwapo na yeye atasalia katika klabu hiyo ya London kaskazini, lakini anasema anafanya kazi ya kuwasajili wachezaji wapya msimu ujao.

Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu na amepewa kandarasi mpya.

''Nafanya kazi hadi siku ya mwisho ya msimu'', alisema Wenger mwenye umri wa miaka 67.

''Wachezaji wanaonunuliwa ndio mpango wa kila klabu katika siku zake za usoni'' ,alisema Wenger.

''Swala la iwapo nitasalia au la sio muhimu kwa sasa, kilicho muhimu ni siku za usoni za klabu hii''.


No comments