WIMBO “MOYO KAMA MACHO” WA KIVURANDE WA KIBAO KATA KUZINDULIWA MAISHA BASEMENT


UONGOZI wa klabu ya Maisha Basement, jijini Dar es Salaam uko katika mazungumzo na mfalme wa Kibao Kata, Kivurande Junior ili kumshawishi kufanyia klabuni hapo uzinduzi wa wimbo wake mpya wa mduara uitwao ‘Moyo Kama Macho’.

Wimbo ‘Moyo Kama Macho’ ambao bado haujaachiwa rasmi, umeibuka kuwa gumzo kubwa hivi sasa kutokana na mashabiki pamoja na wapenzi kuusubiri kwa hamu.

Akiongea na saluti5, Kivurande amesema kuwa wako katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na Maisha Basement ambapo anaamini muda si mrefu mashabiki watatangaziwa tarehe ya uzinduzi wa kibao hicho.

“Nawaomba mashabiki waendelee kutuvutia subira ingawa nafahamu kwamba wana shauku na wimbo huo, mambo yanaenelea kuwa sawa na wakati wowote tutawaeleza siku ya uzinduzi pale Maisha Basement,” amesema Kivurande.

Kivurande anayetikisa kila kona hivi sasa kwa kupagawisha wengi, leo Jumapili ya Pasaka anatarajiwa kuwa mmoja wa wasanii watakaopamba shoo maalum ya ‘Shangwe za Pasaka’ itakayorindima ndani ya ukumbi wa Butiama Chanika, Dar es Salaam.

No comments