WIMBO “MOYO KAMA MACHO” WA KIVURANDE JUNIOR KUZINDULIWA MAISHA BASEMENT

UONGOZI wa klabu ya Maisha Basement, Dar es Salaam uko katika mazungumzo na Mfalme wa Kibao Kata, Kivurande Junior ili kumshawishi kufanyia klabuni hapo uzinduzi wa kibao chake cha mduara cha “Moyo Kama Macho.”

Kibao “Moyo Kama Macho” ambacho bado hakijaachiwa rasmi, kimeibuka kuwa gumzo kubwa hivi sasa kutokana na mashabiki pamoja na wapenzi kukisubiri kwa hamu.

Akiongea na saluti5, Kivurande amesema kuwa wako katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na Maisha Basement ambapo anaamini muda si mrefu mashabiki watatangaziwa tarehe ya uzinduzi wa kibao hicho.

“Nawaomba mashabiki waendelee kutuvuta subira ingawa nafahamu kwamba wana shauku na wimbo huo, mambo yanaendelea kuwa sawa na wakati wowote tutawaeleza siku ya uzinduzi pale Maisha Basement,” amesema Kivurande.

No comments