WISTON KALENGO SASA AKUBALI KUTUA JANGWANI... ajirudisha na kuwaita rasmi Ynga mezani

USAJILI ulioshindikana dirisha la usajili uliopita huenda ukarudi kwa kishindo mwezi mmoja ujao baada ya mshambuliaji raia wa Zambia, Wiston Kalengo kujirudisha rasmi akiwaita mezani Yanga.

Kalengo ambaye alikuwa chaguo la kwanza la kocha George Lwandamina lakini straika huyo akajikuta anasaini FC Leopard ya Congo waliowazidi kete Yanga kwa kumtengea kiasi kikubwa cha fedha.

Taarifa kutoksa ndani ya Yanga zinasema Kalengo anayesifika kwa mashuti ya nguvu na akili kubwa ya kufunga, wiki iliyopita amewapigia simu vigogo wa Yanga akiwataka endapo bado wanamtafuta mshambuliaji yuko tayari kuungana na kocha wake huyo wa zamani.

Bosi mmoja wa Yanga alisema simu hiyo ya Kalengo imewashtua viongozi wenzake ambapo kwanza wanataka kufuatilia uwezo wake kwa sasa kabla ya kufanya maamuzi ya kurudisha mazungumzo hayo.

Kujirudisha huko kwa Kalengo ambaye kikosi chake cha Leapard kimeondolewa katika mashindano ya soka Afrika ni wazi sasa kutaleta vita mpya katika kumpa changamoto kocha Lwandamina kuchagua jina moja kati ya mshambuliaji huyo na Roga Kola ambaye naye alikuwa akipigiwa hesabu.


Endapo Yanga itamsajili mmoja kati ya hao watamuweka katika wakati mgumu Donald Ngoma na Vincent Bossuo ambao inaelezwa kwamba hatua ya kuwapa mikataba mipya itaamuliwa baadaye.

No comments