Habari

YABAINIKA DE GEA ALIPIGWA BENCHI BAADA YA KUMTIBUA MOURINHO

on

DAVID DE GEA alipigwa benchi kwenye mchezo dhidi ya Sunderland  baada ya kupishana lugha na kocha Jose Moirunho – na si kwa sababu ya kuwa majeruhi kama ilivyoripotiwa hapo awali.
Mourinho alisema maumivu ya paja yamepelekea De Gea kuachwa katika mechi hiyo ya ushindi wa 3-0 kwenye dimba la Stadium of Light, lakini sasa The Sun la Uingereza linaipuka na hoja tofauti.
Gazeti hilo linasema vyanzo vyake makini vinadai kiwango kibovu cha De Gea katika mechi za karibuni pamoja kukosoa matamshi ya Mourinho, ndiyo sababu kuu ya nafasi yake kuchukuliwa na Sergio Romelu.
Inasemekana De Gea alichukizwa na kitendo cha Mourinho kuwaponda baadhi ya wachezaji wa Manchester United.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *