YANGA SC: TUKO TAYARI KUMWACHIA MSUVA ASEPE CASABLANKA IKIWA KANUNI ZITAFUATWA

KUFUATIA kuwepo kwa taarifa za klabu ya Wayda Casablanka kufanya mazungumzo na winga Simon Msuva kwa ajili ya kunasa saini yake, uongozi wa Yanga umesema uko tayari kumwachia ikiwa tu kanuni zitafuatwa.

Timu hiyo ilifanya mazungumzo na Msuva wakati Yanga ilipokuwa kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger.

“Hatuna tatizo na Msuva kwenda nje ya nchi, lakini tunahitaji kanuni na taratibu zifuatwe, watuletee barua rasmi ili tukae meza ya mazungumzo kwa ajili ya suala hilo,” alisema Charles Boniface Mkwasa, Katibu wa Yanga.

“Yanga ni klabu kubwa kuliko jina la mchezaji yeyote, hivyo suala la kumzuia Msuva kwa sasa sio mpango wetu, kikubwa ni kufuata taratibu kama kweli wana nia nae maana bado ni mali ya Yanga,” aliongeza Mkwasa.


Nyota huyo amekuwa kwenye kiwango cha juu baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 12 na kuwa kinara katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara.

No comments